15 Machi 2021 - 10:19
Papa aitolea wito jamii ya kimataifa kuijenga upya Syria

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameeleza kusikitishwa na vita haribifu nchini Syria sambamba na kutimia mwaka wa kumi tangu kuanza mgogoro katika nchi hiyo; na kwa mara nyingine tena ametaka kuhitimishwa vita hivyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Papa Francis ameongeza kuwa, vita vya ndani huko Syria vimesababisha moja ya maafa ya kibinadamu katika zama zetu, kuuwa au kujeruhi idadi ya watu isiyofahamika, kupelekea wengine kuwa wakimbizi, mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao, kupotea maelfu ya watu, machafuko ya kila aina, tabu na masaibu makubwa kwa wananchi wote na khususan raia waliodhurika zaidi wakiwa ni watoto, wanawake na wazee. 

Akiwa ziarani hivi karibuni huko Iraq, Papa Francis alitembelea maeneo yaliyovamiwa na wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh na kufanya mazungumzo pia na Ayatullah Sistani Marja Taqlidi wa Waislamu wa Kishia nchini humo.  Marekani ilituma wanajeshi wake kinyume cha sheria huko Syria tangu mwaka 2014 kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh; na wanajeshi wake wangali wapo huko licha ya serikali ya Damascus kuitaka mara kadhaa nchi hiyo iondoe wanajeshi wake huko Syria. Marekani ipo kinyume cha sheria huko Syria kama alivyokiri Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump kwamba, Washington ni chanzo kikuu cha kuibuka makundi mbalimbali ya kigaidi likiwemo lile la Daesh. Ripoti rasmi za Marekani zinaeleza kuwa, hadi sasa nchi hiyo imewapatia magaidi walioko Syria silaha za mabilioni ya dola na zana za kijeshi.  

342/